Baada ya jana usiku katibu mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Nicholas Musonye kutoa onyo kwa Yanga kuwasilisha majina mapya ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya Kagame Cup, leo hii CECAFA wametoa uamuzi mpya dhidi ya Yanga. Yanga SC sasa rasmi imeondolewa kwenye michuano ya Kagame kutokana na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati kupinga kupeleka timu ya vijana. Yanga ilitaka kupeleka timu yenye vijana wengi iliyochanganyika na wakongwe wachache. Lakini Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye akasema hizo ni dharau. Wanasema ni timu ina wachezaji wa timu ya kwanza, vipi Maximo abaki Dar es Salaam. “Halafu timu isafiri kwenda kwenye mashindano makubwa kama ya Kagame. Huu ni utani, ndiyo maana sasa tumeipa nafasi Azam,”alisema jana. Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC, watapambana Kundi A lenye timu za Rayon Sport ya Rwanda, Coffee ya Ethiopia, Atlabara ya Sudan Kusini na KMKM ya Zanzibar....
Comments
Post a Comment