SIMULIZI FUPI YA KUSISIMUA TAMAA IMENIPONZA KWELI KWELI.......!!
MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE Ritha alikuwa ni msichana mrembo sana, kila aliyemtizama alivutiwa na urembo alionao, na hata yeye alijitambua kuwa ni mrembo. Katika maisha yake Ritha alikuwa anapenda sana vitu vizuri na vinavyokwenda na wakati kama nguo, viatu, simu na vitu vingine kadha kwa kadha. Lakini wazazi wake walikuwa hawana uwezo wa kumnunulia vitu vyote hivyo. Baada ya kumaliza kidato cha nne, kwa bahati mbaya hakufanikiwa kuendelea na kidato cha sita na hivyo wazazi wake waliamua kumtafutia chuo.Akiwa anasoma chuo alikutana na marafiki wa aina mbalimbali na marafiki zake wakubwa walikuwa ni wale ambao wametokea katika familia ambazo wanajiweza yaani matajiri. Kutokana na wazazi wao kuwa na pesa walikuwa wakimiliki simu nzuri, na kompyuta (laptop) lakini kwa upande wa Ritha alikuwa hana hata simu ya mkononi, alitamani sana kuwa na maisha mazuri kama ya wenzake. Siku moja akiwa anatoka chuo kuelekea nyumbani alikutana kaka mmoja aliy...
Comments
Post a Comment